NAFASI 1500 za Walimu wa Kujitolea Shuke za Sekondari 2026

Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM –TAMISEMI)
kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu “Global Partnership for Education Teacher
Support Programme(GPE – TSP)” inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuratibu
upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea (engagement of volunteer teachers).
Kupitia mradi huu, OWM – TAMISEMI inatangaza nafasi za kujitolea kwa walimu 1,500
wa Shule za Sekondari zilizopo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye uhitaji
mkubwa zaidi kwa kuzingatia utaratibu wa kupanga walimu wa Shule za Sekondari
(Secondary Teacher Allocation protocol (S – TAP).
Hivyo OWM – TAMISEMI kupitia mradi wa GPE – TSP inawaalika Watanzania wenye sifa
kuwasilisha maombi ya nafasi elfu moja na mia tano (1,500) za Ualimu wa Kujitolea
kama zilivyoainishwa katika tangazo hili. Nafasi hizi zinalenga walimu wa masomo ya
Sayansi na Teknolojia (STEM), Masomo ya Amali (Vocational Subjects) na Masomo ya
Biashara (Business Studies).
NAFASI 1500 za Walimu wa Kujitolea Shuke za Sekondari 2026
Bonyeza Hapa Kudownload PDF ya Tangazo
